Thursday, May 21, 2015

Jinsi ya kumuogesha mtoto mchanga: How to give bath to a new born

Habari,

Naamini wiki hii ni njema kwako. Namshukuru Mungu kuwa ni njema kwangu pia. Siku ya pili baada ya kujifungua niliuliza lini nitaanza kumuogesha mtoto wangu. Mmmh, niliambiwa niache haraka. Lakini pia nakumbuka kuwa kuna wamama ambao wanakuwa waoga sana kuwaogesha watoto wanapokuwa wadogo sana, sio kosa ni hali ya kawaida. Nilipata tips kadhaa kutoka kwenye video katika mtandao wa Baby Center na nilipata confidence wakati ulipofika wa kumuogesha mtoto wangu.

Leo nitakushirikisha vitu vichache vya kufanya unapomuogesha mtoto, ila kabla ya hayo ni muhimu kukumbuka kuwa:
Image result for how to bathe a newborn for the first time

  • Mtoto hapaswi kuogeshwa ndani ya beseni kabla kitovu hakijakatika na kukauka kabisa
  • Si lazima mtoto chini ya mwaka mmoja (1) kuogeshwa kila siku, mara tatu kwa wiki inatosha.
  • Usitumie sabuni ya kunukia au zile za brand kubwa kama Baby Johnson mapema hii ni kuepuka allergies, tumia sabuni ya kufulia au "Mild soap"
  • Kutokana na kutozoea maji ni kawaida mtoto kulia wakati wa kuoga ila wengine wanakua hawana tatizo
Haya vidokezo hivi 7 vitakusaidia kupata ujuzi wa swala hili nyeti
  1. Kusanya mahitaji yote ya kutumia, taulo safi litandaze kitandani, nepi au diaper, mafuta kitana na nguo. Hakikisha chumba kina joto la kutosha ili mtoto asipate ubaridi (unaweza kuwasha taa dakika kama 15 kabla ya kumuogesha mtoto, jiko la mkaa wachache hutumia ila si salama sana. Waweza kuliweka ndani likiwa halina harufu na kabla hujamleta mtoto kuoga litoe ili mtoto asivute hewa ya mkaa)
  2. Weka maji kwenye karai, yasizidi kama inchi 3 hivi, yasiwe ya moto yawe ya uvuguvugu. Tumia kiwiko cha mkono kuangalia joto la maji. Unaweza kuweka nguo safi ya pamba kama taulo ndani ya karai ilikuzuia mtoto kuteleza unapomwogesha.
  3. Mlete mtoto eneo la kumuogeshea na mvue nguo zote ila kama ni muoga sana wa maji muachie nepi ili ajisikie salama
  4. Mwingize mtoto kwenye beseni taratibu kwa kuanza na miguu. mmiminie maji mara kwa mara ili asipate baridiImage result for how to bathe a newborn for the first time
  5. Muogeshe mtoto na mikono au kitambaa laini na usitumie sabuni nyingi sana maana ngozi itakauka sana. Osha kichwa kwanza halafu uso, macho na pua. Anzia mbele kuelekea mgongoni. Mwoshe sehemu za siri vizuri na usitumie sabuniImage result for how to bathe a newborn for the first time
  6. Msuuze mtoto , mnyanyue mtoto taratibu hakikisha umemshika vizuri maana anateleza. Mkono mmoja weka eneo la shingo ili apate support. Muweke kwenye lile taulo uliloliandaa awaliImage result for how to bathe a newborn for the first time
  7. Mkaushe mtoto kwa jinsi ya "ku-pat" kama vile unamkanda taratibu usimfute, usitumie nguvu, kama ngozi inatoka paka mafuta ya watoto, mafuta ya nazi ni mazuri sana. Baada ya hapo mvishe nguo, mkumbatie na ummpe busu kichwani. 

http://www.babycenter.com/2_how-to-give-your-newborn-a-bath_1486858.bc. Video hii ilikuwa msaada sana kwangu.

Happy parenting.

ATM

No comments: